28 Juni 2015 - 20:41
Wanamgambo 20 wa Taliban wauwawa Pakistan

Shirika la habari la ABNA linatuarifu kuwa: Maafisa wa idara ya ujasusi nchini Pakistan wamesema shambulizi la anga lililofanywa na vikosi vya usalama, limewauwa takriban watu 20 wanaotuhumiwa kuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la Taliban.

Shirika la habari la ABNA linatuarifu kuwa: Maafisa wa idara ya ujasusi nchini Pakistan wamesema shambulizi la anga lililofanywa na vikosi vya usalama, limewauwa takriban watu 20 wanaotuhumiwa kuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la Taliban. Shambulizi hilo limefanywa kaskazini magharibi mwa nchi hiyo katika bonde la Shawal leo hii, ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja tangu vikosi hivyo kuvamia maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo.

Maafisa wawili wa idara ya ujasusi ambao hawakutaka kutajwa kwa majina, wamesema shambulizi hilo limetokea katika eneo la Zoirani kaskazini mwa Waziristan.

Eneo hilo la Waziristan lilikuwa linadhibitiwa lote na kundi la itikadi kali za kiislamu la Taliban, lakini sasa vikosi vya usalama vimefanikiwa kuzikomboa sehemu nyingi likiwamo eneo la bonde la Shawal, tangu kuanza kwa operesheni hiyo Juni mwaka uliopita.

Mwisho wa habari/ 291